Uchunguzi wa awali unaashiria kwamba mgonjwa wa kwanza wa virusi hivyo huenda alipata dalili za maambukizi hapo mwezi Agosti lakini hakukutambua alikuwa anaugua ebola.
Watu 24 wamethibitishwa kuambukizwa Ebola aina ya Sudan. Watu wanne wamefariki.
Dalili za virusi vya Ebola aina ya Sudan zinafanana na dalili za maambukizi ya malaria na homa ya tumbo, ambayo ni magonjwa yanayotokea katika mara katika sehemu ambazo ebola umeripotiwa Uganda na hivyo kuwa vigumu kwa madaktari kugundua ebola kwa haraka.
Hakuna chanjo dhidi ya virusi vya Ebola aina ya Sudan