Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 04:00

White House yasisitiza Comey alistahili kufukuzwa


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Ikulu ya White House siku ya Alhamisi imeendelea kutetea jinsi ilivyoshughulikia suala la kuachishwa kazi kwa mkurugenzi wa makosa ya jinai (FBI), katikati ya uchunguzi uliokuwa unaendelea wa madai juu ya mafungamano kati ya kampeni ya uchaguzi wa rais mwaka jana na maafisa wa Russia.

Katika kielele cha uchunguzi huo pia inaangaliwa iwapo naibu mwanasheria mkuu wa Idara ya Sheria, Rod Rosenstein, alikuwa ameamrishwa kuandaa nyaraka inayohalalisha kuondolewa kwa Mkurugenzi wa FBI James Comey au aliamua kuandika waraka huo bila ya kuagizwa kufanya hivyo.

Rosenstein alikuwa amekasirishwa na maelezo ya White House kwamba waraka wake ulikuwa umependekeza kuwa Comey afukuzwe kazi, kwa mujibu wa gazeti la Washington Post na shirika la habari la ABC.

Maafisa wa White House siku ya Alhamisi walikanusha kuwepo mjadala wowote kwa upande wa Rosenstein, wakisema kuwaambia waandishi kuwa mwendesha mashtaka wa siku nyingi alikuwa ameandaa yeye mwenyewe waraka huo na sio kwamba alihimizwa kwa kupewa amri na Rais Donald Trump.

Rais anategemewa kutembelea makao makuu ya FBI pengine haraka Ijumaa, kwa mujibu wa maafisa wa White House. Trump alimtumia Comey barua Alhamisi kumfahamisha kuwa amefutwa kazi.

Nyaraka ya Rosenstein na ya Mwanasheria Mkuu General Jeff Sessions zilizotumwa na barua hiyo ya kumwachisha kazi zilitaja kuwa Comey alifanya makosa katika uchunguzi wa mwaka jana wa mgombea wa chama cha Demokratik Hillary Clinton juu ya kutumia server ya barua pepe binafsi wakati akiwa waziri wa mambo ya nje.

Vyombo vya habari hata hivyo vimekuwa vikinukuu vyanzo vya habari Washington vikisema kuwa Comey aliondolewa kwa ghafla kwa sababu alikuwa anataka kuendeleza uchunguzi wa kina dhidi ya Russia.

Kufukuzwa kwake kumesababisha Wademokrati kupaza sauti zao wakitaka uchunguzi wa kujitegemea ufanyike katika suala la Russia.

Waraka wa Rosenstein ni “waraka wa kisiasa” ambao unaonekana “uliandaliwa kwa haraka kuhalalisha kufikia maamuzi hayo yaliyokuwa yameshapangwa,” amesema Seneta Dianne Feinstein, Mdemokrati wa ngazi ya juu katika kamati ya sheria, katika tamko lililotolewa Alhamisi.

Wademokrati katika Baraza la Seneti wanasema kuwa wanatafuta maelezo zaidi kutoka Idara ya Sheria iwapo Comey, kabla ya kufukuzwa madarakani, aliomba fedha zaidi na wafanyakazi zaidi kwa ajili ya kuendeleza uchunguzi wa mahusiano ya Russia.

Baadhi ya Warepublikan pia wameeleza wasiwasi wao kuhusu muda na sababu za kuondolewa kwa ghafla Comey katika nafasi yake.

Maafisa wa White House wamesema kuwa Trump alikuwa anafikiria namna ya kumfukuza Comey tangu mwaka jana Novemba wakati wa uchaguzi.

XS
SM
MD
LG