Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 17:33

WFP yasitisha operesheni ya usambazaji chakula Ethiopia


WFP ikigawa msaada wa chakula kaskazini mwa Ethiopia
WFP ikigawa msaada wa chakula kaskazini mwa Ethiopia

WFP ilisema wameiba kiasi kikubwa cha chakula ikiwa ni pamoja na kile cha watoto wenye utapiamlo. Kaskazini mwa Ethiopia kuna janga kubwa la njaa kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea baina ya wapiganaji wa Tigray na vikosi vya serikali

Shirika la Mpango wa chakula duniani (WFP) limesitisha msaada wa usambazaji wa chakula katika miji miwili ya Ethiopia baada ya watu waliokuwa na silaha kupora katika ghala zake. Waporaji kutoka vikosi vya Tigray waliwashikilia wafanyakazi wa misaada wakiwa wamewaelekezea bunduki katika mji wa Kombolcha, Umoja wa Mataifa ulisema.

Wameiba kiasi kikubwa cha chakula ikiwa ni pamoja na kile cha watoto wenye utapiamlo. Kaskazini mwa Ethiopia kuna janga kubwa la njaa kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea baina ya wapiganaji wa Tigray na vikosi vya serikali. Baada ya mapigano ya zaidi ya mwaka mmoja watu zaidi ya milioni tisa wako katika shida kubwa ya chakula, Umoja wa Mataifa ulisema. Msemaji wa UN ambayo inasimamia WFP alisema wafanyakazi wake wamekabiliwa na vitisho vikubwa wakati wa siku za uporaji.

WFP katika harakati za kugawa chakula huko Gondar, Ethiopia, Sept. 15, 2021.
WFP katika harakati za kugawa chakula huko Gondar, Ethiopia, Sept. 15, 2021.

Alisema unyanyasaji huo kwa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu unaofanywa na vikosi vyenye silaha haukubaliki. Unadumaza uwezo wa Umoja wa Mataifa na washirika wake wa kibinadamu kusaidia kusambaza chakula wakati kinahitajika zaidi. Msemaji huyo pia amevishutumu vikosi vya serikali kuamuru kusitishwa magari makubwa matatu ya WFP ya misaada ya kibinadamu na kutumia kwa manufaa yao wenyewe. Hali hiyo imesababisha kusitishwa usambazaji wa chakula huko Kombolcha na eneo jirani la Dessie, miji miwili ya kimkakati katika mkoa wa kaskazini wa Amhara ulioko katika barabara inayoelekea mji mkuu wa Addis Ababa.

Vikosi vya Tigray havijatoa maelezo yoyote kwamba wapiganaji wake wameiba chakula cha msaada. Hivi karibuni serikali ya Ethiopia ilitangaza kwamba imekomboa tena miji kutoka kwa wapiganaji wa Tigray.

XS
SM
MD
LG