Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:48

Waziri wa zamani wa fedha wa Msumbiji akamatwa


Manuel Chang, waziri wa zamani wa fedha Msumbiji
Manuel Chang, waziri wa zamani wa fedha Msumbiji

Chang alikuwa anatafutwa kwa shutuma za njama za kutenda wizi kwa njia ya mtandao, njama nyingine za wizi wa dhamana za kifedha na biashara haramu ya mzunguko wa fedha

Waziri wa zamani wa fedha wa Msumbiji, Manuel Chang amekamatwa nchini Afrika kusini kwa ombi la Marekani msemaji wa polisi Afrika kusini Vish Naidoo alisema siku ya Jumatatu.

Chang alikuwa anaongoza wizara ya fedha wakati wizara ilipotoa dhamana ya kukopesha kwa siri dola bilioni 2 kwa makampuni yanayomilikiwa na serikali mwaka 2013 na 2014 kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters alikamatwa Jumamosi mjini Johannesburg alikuwa anatafutwa na Marekani.

Manuel Chang
Manuel Chang

Wakati huo huo shirika la habari la Msumbiji lilisema Chang mwenye miaka 63 alikuwa anatafutwa kwa shutuma za njama za kutenda wizi kwa njia ya mtandao, njama nyingine za wizi wa dhamana za kifedha na biashara haramu ya mzunguko wa fedha. Ilisema mashtaka hayo hayahusiani na suala la ukopeshaji wa siri ambayo ulichochea wafadhili wa kigeni ikiwemo IMF kukata msaada wa fedha na kusababisha sarafu ya nchi kuanguka na nchi kushindwa kulipa madeni.

XS
SM
MD
LG