Waziri wa usalama wa ndani hapa Marekani Alejandro Mayorkas na gavana wa Texas Greg Abbott wamezozana jumapili juu ya utekelezaji wa sheria za uhamiaji za nchi baada ya maelfu ya wahamiaji wa Haiti kulundikana na kisha kuondolewa kutoka kwenye mji ulio kwenye mpaka wa Marekani na Texas, Del Rio.
Katika mahojiano kwenye kipindi cha televisheni cha Fox news Sunday , Mayorkas alitetea jinsi serikali ilivyochukua hatua kutokana na vurugu zilizotokea katika mpaka kulingana na sheria za serikali kuu na kwa kile alichosema kuwa ni moja wa “utamatuni wa kujivUnia” wa kuruhusu wahamiaji kuingia Marekani kutafuta hifadhi na usalama wakikimbia hali mbaya kwenye nchi zao.
Kuhusu Abbott, mkosoaji wa muda mrefu wa Washington kwa majibu yake kuhusu maelfu ya wahamiaji wa Haiti na Amerika ya kati , akisema kuwa Mayorkas na rais Joe Biden wameachana na ulinzi wa mpakani na badala yake wametuma ujumbe katika dunia kwamba mpaka uko wazi.
Abbott alizungumza katika mahojiano tofauti kwenye program hiyo hiyo. Karibu raia 30,000 wa Haiti walikusanyika katika mpaka huo kwa kipindi cha siku 17 kuanzia September 7. Wakati maelfu ya raia wa Haiti wanarejea Mexico, marekani imewarejesha zaidi ya 2000 kwa kutumia ndege katika taifa hilo la carribean.