“Ninaposema kwamba jambo kama hili haliwezi kutokea, tunazungumzia uzembe,” waziri wa usalama wa ndani Alejandro Mayorkas alikiambia kituo cha televisheni cha CNN.
“Tutachunguza kupitia ukaguzi huru, jinsi jambo hilo lilitokea, na kutoa mapendekezo na matokeo ili kuhakikisha kuwa halijirudii tena. Nimeliweka wazi zaidi.”
Mayorkas alikiambia kituo cha televisheni cha ABC news katika mahojiano mengine kwamba haingewezekana mshambuliaji aliyetambulishwa kwa jina la Thomas Matthew, mwenye umri wa miaka 20 amfyatulie risasi nyingi Trump kwa kutumia silaha nzito kama alivyofanya akiwa kwenye paa ya nyumba ya jengo lililokuwa karibu.
Mshambuliaji alifyatua risasi akiwa umbali wa mita 150 na mahali ambapo rais wa zamani alikuwa akihutubia wafuasi wake Jumamosi jioni katika mji mdogo wa Pennsylvania wa Butler.
Forum