Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:08

Waziri wa mambo ya nje wa Thailand afanya ziara Qatar na Misri kwa lengo la kutaka Hamas iwaachiye huru mateka 22 wa Thailand


Watu wakishikilia mabango yenye picha za mateka wanaoshikiliwa na Hamas wakikusanyika nje ya ubalozi wa Qatar mjini London, Oktoba 29,2023.
Watu wakishikilia mabango yenye picha za mateka wanaoshikiliwa na Hamas wakikusanyika nje ya ubalozi wa Qatar mjini London, Oktoba 29,2023.

Waziri wa mambo ya nje wa Thailand leo Jumanne ameanza ziara ya dharura nchini Qatar na Misri kwa ajili ya mazungumzo juu ya hatma ya raia 22 wa Thailand wanaoshikiliwa mateka na Hamas wakati wa shambulio la kundi hilo nchini Israel.

.Mamlaka za Israel zinasema zaidi ya watu 1,400, wengi wao wakiwa raia, waliuawa katika shambulio lililofanywa na kundi hilo la wanamgambo wa Palestina tarehe 7 Oktoba wakitokea Ukanda wa Gaza.

Kujibu, jeshi la Israel limeshambulia Gaza, ambako wizara ya afya inayodhibitiwa na Hamas inasema zaidi ya watu 8,300 wameuawa, zaidi ya 3,000 kati yao ni watoto.

Zaidi ya mateka 230 wanashikiliwa na Hamas huko Gaza, kulingana na takwim za hivi karibuni za Israel, 22 kati yao ni raia wa Thailand, wizara ya mambo ya nje mjini Bangkok imesema.

Hata hivyo, maafisa wa Israel wamesema raia 54 wa Thailand ni miongoni mwa mateka.

Waziri mkuu wa Thailand Srettha Thavisin jana Jumatatu alisema serikali yake inafanya kazi kwa bidi kuwarejesha nyumbani raia wa Thailand.

Forum

XS
SM
MD
LG