Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 15:15

Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway atoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufanyia kazi suluhisho  la mataifa mawili

Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Espen Barth Eide, wa pili kushoto, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan, Ayman Safadi, wa pili kulia, wakati wa mkutano kwenye jengo la Baraza la Ulaya mjini Brussels, Jumatatu, Mei 27, 2024.AP.

Uhispania na Norway zililitambua taifa la Palestina Jumanne, huku Ireland ikitarajiwa kufuatia, wakijiunga na mataifa mengine zaidi ya 140 katika hatua iliyokosolewa  vikali na Israel.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Espen Barth Eide alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufanyia kazi suluhisho la mataifa mawili, huku akiipongeza Mamlaka ya Palestina kwa kufanya mageuzi na kuilaumu serikali ya Israel kwa kutoonyesha dalili zozote za kujihusisha kikamilifu.

Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sánchez alisema Jumanne kwamba kulitambua taifa la Palestina kunalenga katika "kuchangia kupatikana kwa amani kati ya Waisraeli na Wapalestina."

Forum

XS
SM
MD
LG