Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen amewasili Beijing leo alhamisi kwa ziara ya siku nne nchini China.
Yellen antarajiwa kukutana na maafisa wa China na pande zote mbili zinatarajiwa kufanya mazungumzo kuhusu uchumi, maswala ya biashara, na uhusiano kati ya China na Marekani.
Ziara hiyo itakayomalizika jumapili, inajiri wiki chache baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken kutembelea China.
Forum