Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 17:23

Waziri mteule wa fedha huko Kenya atetea jukumu la IMF nchini humo


Bendera ya Kenya
Bendera ya Kenya

IMF kamwe haijawahi kujialika nchini. Tunawaalika wao na kukubaliana na program yao, John Mbadi aliliambia Jopo la bunge.

Waziri mteule wa Fedha wa Kenya John Mbadi, leo Jumamosi alitetea jukumu la shirika la kimataifa la fedha duniani-IMF katika kusaidia uchumi wa Kenya kwa sasa, lakini alisema nchi inatakiwa kujiongezea kipato zaidi kwa kupunguza nakisi ya bajeti yake na kuhamia kwa deni nafuu.

Taifa hilo la Afrika Mashariki, ambalo limekumbwa na maandamano yaliyokuwa yakipinga ongezeko la kodi katika kipindi cha miezi miwili iliyopita yakitoa wito kwa Rais William Ruto aachane na mpango wa bajeti wa mwaka huu, aliridhia program ya mkopo na shirika hilo la fedha lenye makao yake washington mwaka 2021, ambapo tangu wakati huo imekua na kupanuka.

IMF kamwe haijawahi kujialika nchini. Tunawaalika wao na kukubaliana na program yao, John Mbadi aliliambia Jopo la bunge.

Hata hivyo Mbadi alisema hafikirii Kenya inahitaji kuwa chini ya program ya IMF kwa muda mrefu. Lazima tuhamie kwenye mfumo ambao tunafanya mageuzi wenyewe kutoka kwa IMF, na kuanza kujitegemea sisi wenyewe.

Forum

XS
SM
MD
LG