Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 01:09

Waziri mkuu wa Uingereza Johnson, anusurika katika kura ya kutokuwa na imani naye


Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson akiondoka kwenye ofisi yake kuhudhuria kikao cha masuali cha kila wiki cha Bunge la Uingereza, mjini London, May 25, 2022. Picha ya AP
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson akiondoka kwenye ofisi yake kuhudhuria kikao cha masuali cha kila wiki cha Bunge la Uingereza, mjini London, May 25, 2022. Picha ya AP

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson Jumatatu amenusurika katika kura ya bunge ya kutokuwa na imani naye, lakini upinzani mkubwa katika chama chake cha Conservative, umedhoofisha mamlaka yake, kufuatia kashfa ya kufanya sherehe wakati wa masharti makali ya kupambana na covid.

Johnson ambaye alipata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa 2019, amekuwa chini ya shinikizo kubwa baada ya yeye na wafanyakazi wake kuanda sherehe ya kunywa pombe kwenye ofisi yake ya Downing street na nyumbani kwake wakati Uingereza ilikuwa chini ya masharti makali ya kukabiliana na janga la Covid 19.

Wabunge kadhaa wamesema, kuona wabunge 211 ndio walimuunga mkono na 148 wakapiga kura ya kumpinga, ni ishara mbaya kuliko ilivyokuwa inatarajiwa kwa waziri mkuu.

“Boris Johnson amepata afueni kwenye kura hii, lakini anatakiwa pia kuelewa kwamba kipaumbele cha kufuata ni kujenga umoja kwenye chama chake, David Jones, waziri mkuu wa zamani ameiambia Reuters.

Kwa kushinda kura ya kuwa na imani naye, Johnson amepata afueni kwa miezi 12 ambapo wabunge hawawezi kuleta changamoto nyingine.

Baada ya kura hiyo, Johnson amesema hana mpango wa kuitisha uchaguzi wa kitaifa wa haraka.

“Nadhani ni matokeo ya kuridhisha kwa siasa na nchi, ni matokeo madhubuti na maana yake ni kwamba kama serikali tunaweza kuendelea na kujikita kwenye mambo ambayo nadhani ni muhimu kwa wananchi,” amemwambia mwandishi wa habari.

XS
SM
MD
LG