Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 06:34

Waziri Mkuu wa Sri Lanka akubali kujiuzulu baada ya waandamanaji kuvamia makazi ya Rais


Waandamanji wavamia makazi rasmi ya Rais Gotabaya Rajapaksa mjini Colombo, Sri Lanka, wakimtaka yeye na serikali yake kujiuzulu.
Waandamanji wavamia makazi rasmi ya Rais Gotabaya Rajapaksa mjini Colombo, Sri Lanka, wakimtaka yeye na serikali yake kujiuzulu.

Waziri Mkuu wa Sri Lanka alikubali kujiuzulu Jumamosi baada ya viongozi wa chama katika bunge kumtaka yeye na rais kuondoka madarakani katika siku ambayo waandamanaji walivamia makazi na afisi ya rais kuelezea hasira yao juu ya mzozo mbaya wa kiuchumi unaloikumba nchi hiyo.

Msemaji wa Waziri Mkuu, Dinouk Colambage, alisema Ranil Wickre-mesinghe aliwaambia viongozi wa chama kwamba atajiuzulu wakati pande zote zikikubaliana juu ya kuundwa kwa serikali mpya.

Uamuzi wake ulikuja baada ya maandamano makubwa zaidi Jumamosai, ambapo maelfu ya watu wakivuka vizuizi na kuingia katika makazi ya Rais Gotabaya Rajapaksa na afisi iliyo karibu ili kuonyesha hasira zao dhidi ya kiongozi wanayesema amesababisha mzozo mbaya zaidi wa kitaifa.

Awali msemaji wa rais huyo alisema alikuwa amepelekwa mahali salama, naye afisa mmoja mwandamizi wa ulinzi katika serikali ya Sri Lanka akisema "rais amesindikizwa na kupelekwa mahali salama."

Maafisa wa usalama walifyatua risasi hewani ili kujaribu kuwazuia waandamanaji kuwazidi nguvu na kuliteka kasri la rais, ila mwishowe waandamanaji hao walifanikiwa na kuwazidi nguvu. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP Waziri Mkuu Ranil Wick-reme-singhe aliitisha mkutano wa dharura wa wakuu wa vyama vya kisiasa, kufuatia sintofahamu hiyo ya Jumamosi.

Hali kadhalika alitoa wito kwa spika kuitisha kikao cha bunge cha dharura, ilisema taarifa kutoka afisi ya waziri mkuu.

Kisiwa cha Sri Lanka kinakabiliwa na mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi tangu kilipopata uhuru mwaka 1948, huku rais wake amekataa kujiuzulu.

Katika kile kinachoonekana na wachambuzi kama hatua ya kutaka kuwaridhisha waandamanaji, rais huyo amewaachisha kazi jamaa zake kadhaa waliokuwa wanashikilia nyadhfa za juu serikalini, wakiwemo ndugu zake wawili waliokuwa wanahudumu kama waziri mkuu na waziri wa fedha. Hata hivyo, hilo halijaonekana kama lililowashawishi wapinzani wake.

Tariban raia milioni 22 wa Sri Lanka wanakabiliwa na mfumko wa bei unaozidi kwa miezi kadhaa pamoja na muda mrefu wa kukosekana kwa nguvu za umeme baada ya serikali kukosa fedha za kigeni za kununua bidhaa kama chakula, mafuta na dawa.

XS
SM
MD
LG