Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 21, 2024 Local time: 12:03

Waziri Mkuu wa Mauritius amekubali muungano wake unaelekea kushindwa


Waziri Mkuu wa Mauritius Pravind Kumar Jugnauth wakati wa upigaji kura uliofanyika Nov. 10, 2024. (Rishi Etwaroo/L'Express Maurice/AFP)
Waziri Mkuu wa Mauritius Pravind Kumar Jugnauth wakati wa upigaji kura uliofanyika Nov. 10, 2024. (Rishi Etwaroo/L'Express Maurice/AFP)

Matokeo ya mwisho bado hayajatolewa lakini kiongozi wa upinzani Navin Ramgoolam anaonekana kuwa waziri mkuu kwa mara ya tatu

Waziri Mkuu wa Mauritius Pravind Jugnauth amekubali leo Jumatatu kwamba muungano wake unaelekea katika hali ya kusuasua katika uchaguzi wa bunge unaozozaniwa na kuzusha njia kwa upinzani kuchukua madaraka.

Matokeo ya mwisho katika upigaji kura wa Jumapili bado hayajatolewa, lakini kiongozi wa upinzani Navin Ramgoolam anaonekana kuwa waziri mkuu kwa mara ya tatu katika uongozi wa muungano wake wa Alliance of Change.

Jugnauth alisema muungano wake wa Lepep, ukiongozwa na chama chake cha Militant Socialist Movement (MSM), unaelekea kushindwa kwa kiasi kikubwa, baada ya uchaguzi uliofanyika katika moja ya demokrasia imara na yenye mafanikio barani Afrika.

Watu wamechagua timu nyingine ya kuongoza nchi, Jugnauth, ambaye amekuwa waziri mkuu wa taifa hilo lililoko katika kisiwa cha Bahari ya Hindi tangu 2017 aliwaambia waandishi wa habari.

Forum

XS
SM
MD
LG