Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 17:02

Waziri mkuu wa Japan amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri


Waziri mkuu wa Japan, Fumio Kishida, Jumatano amefanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri na nafasi muhimu katika chama ili kuimarisha  nafasi yake kabla ya uchaguzi muhimu wa chama mwaka ujao  ambapo amemteua waziri wa ulinzi na mambo ya nje mwanamke kwa mara ya kwanza toka mwaka 2004.

Waziri mkuu Kishida ameteua wanawake watano katika baraza lenye mawaziri 19, ikiwa ni sehemu ya kujaribu kupata uuganji mkono baada ya kuachana na baraza lake lililokuwa na mawaziri wengi wanaume na wanawake wawili tu.

Wanawake hao watano wanakuwa idadi sawa na wale waliokuwepo kwenye baraza la mawaziri la mwaka 2014 na 2001.

Haya ni mabadiliko ya pili ya baraza la mawaziri toka waziri mkuu Kishida aingie madarakani Oktoba 2021.

Forum

XS
SM
MD
LG