Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 21:31

Waziri Mkuu wa Israel anafanya ziara kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu


Waziri Mkuu wa Israel, Naftali Bennett
Waziri Mkuu wa Israel, Naftali Bennett

Safari hiyo inakuja huku kukiwa na hali ya mvutano wa kikanda, wakati mataifa yenye nguvu duniani yakijaribu kufufua mkataba wa nyuklia na Iran. Israel na baadhi ya mataifa ya kiarabu ya ghuba wanaelezea wasi wasi wao kuhusu harakati  za Iran katika eneo hilo

Waziri Mkuu wa Israel, Naftali Bennett anasafiri kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu leo Jumapili na kukutana na mtawala mkuu wa nchi hiyo ya ghuba, katika ziara hiyo ya ngazi ya juu zaidi, tangu nchi hizo ziliporasmisha uhusiano mwaka jana.

Safari hiyo inakuja huku kukiwa na hali ya mvutano wa kikanda, wakati mataifa yenye nguvu duniani yakijaribu kufufua mkataba wa nyuklia na Iran. Israel na baadhi ya mataifa ya kiarabu ya ghuba wanaelezea wasi wasi wao kuhusu harakati za Iran katika eneo hilo. Nitaondoka leo kwenda Umoja wa Falme za kiarabu katika ziara ya kwanza kuwahi kufanywa na Waziri Mkuu wa Israel, Bennett aliuambia mkutano wa baraza lake la mawaziri siku ya Jumapili. Hakukuwa na uthibitisho wa haraka kutoka Abu Dhabi.

Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na Bahrain, Sudan na Morocco zilielekea katika kuwa na uhusiano wa kawaida na Israel chini ya mpango uliofadhiliwa na Marekani, uliojulikana kama “Abraham Accords” kuelezea kama baba mkuu wa kibiblia, anayeheshimiwa na Wayahudi, Wakristo na Waislam.

Naftali Bennett, Waziri Mkuu wa Israel. Aug. 18, 2021 in Jerusalem. (Abir Sultan/Pool Photo via AP)
Naftali Bennett, Waziri Mkuu wa Israel. Aug. 18, 2021 in Jerusalem. (Abir Sultan/Pool Photo via AP)

Safari ya Bennett ya Jumapili itakuwa ya kwanza kwa Waziri Mkuu wa Israel katika nchi yoyote kati ya hizo nne. Safari zilipangwa na mtangulizi wake na aliyetia saini wa Mkataba wa Abraham, Benjamin Netanyahu zilifutwa, huku Israel ikieleza kusitisha safari wakati wa COVID-19, na pia vigumu kupanga safari za ndege kupita katika anga ya Jordan.

Bennett atakutana na mwanamfalme wa Abu Dhabi, Sheikh Mohammed bin Zayed al-Nahyan, hapo kesho Jumatatu, ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel ilisema. Viongozi hao wawili watajadili kuimarika kwa uhusiano wao huku wakitilia mkazo katika masuala ya kiuchumi ambayo yatachangia mafanikio, ustawi na kuimarisha utulivu kati ya nchi hizo mbili, taarifa ya Israel iliongeza.

XS
SM
MD
LG