Ziara ya Li inafanyika wakati China na Russia, zikiimarisha ushirikiano wa kiuchumi na mawasiliano ya kidiplomasia.
“Chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu hao wawili wa nchi, uhusiano kati ya China na Russia umeondoa uingiliwaji wa nje na kudumisha maendeleo yenye tija na utulivu,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Mao Ning aliumbia mkutano wa vyombo vya habari.
Amesema katika taarifa yake kwamba ziara ya Li kuanzia leo Jumanne mpaka Ijumaa, itajumuisha mkutano wa 29 wa kawaida kati ya wakuu wa serikali wa China na Russia.
Mao amesema Li amepanga kufanya mazungumzo ya kina juu ya ushirikiano wa kivitendo katika kwa nchi hizo mbili akiwa na mwenzake wa Russia, Mikhail Mishustin.
Forum