Wanawake wawili waliuawa na mtoto mmoja alijeruhiwa vibaya wakati kilipuzi kilipolipuka wakati punda wao alipokuwa akipita karibu na Bosso, katika eneo la Diffa, karibu na Nigeria, mkazi wa eneo hilo alisema.
Afisa wa mkoa alithibitisha kuwa watu wawili walikufa, bila kutoa maelezo zaidi.
Bosso, katika mwambao wa Ziwa Chad, maeneo ambayo hushambuliwa mara kwa mara na wanajihadi, ikiwa ni pamoja na Boko Haram na mpinzani wake, kundi la Islamic State La Afrika magharibi (ISWAP).
Mwezi uliopita, washukiwa wa wanajihadi wa Boko Haram waliwaua wakulima 11 huko Diffa, afisa wa eneo hilo alisema.
Niger, nchi maskini zaidi duniani kwa kigezo cha orodha ya Maendeleo ya Binadamu ya Umoja wa Mataifa, imeathirika kwa kiasi kikubwa na uasi ulioanza kaskazini mwa Mali mwaka 2012.