Wawakilishi wa NATO wanafikiria namna ya kuijibu Syria kwa kuangusha ndege ya kijeshi ya Uturuki wiki iliyopita.
Uturuki iliomba mkutano Jumanne huko Brussels kufuatia shambulizi wanalosema lilitokea kwenye anga ya kimataifa. Syria wanasema tukio hilo ni kitendo cha kujilinda.
Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa kutoa maelezo zaidi kwa majibu ya nchi yake jumanne wakati wa hotuba kwa watunga sheria bungeni.
Naibu Waziri Mkuu Bulent Arinc amesema Uturuki haitaki kwenda vitani kutokana na tukio hilo lakini ina haki ya kulipa kisasi kutokana na sheria ya kimataifa.
Wakati huo huo kutokana na wito wa NATO, Uturuki imelaani shambulizi la Ijumaa kwenye barua yake kwa Umoja wa mataifa wakisema kitendo hicho kinaleta hatari kubwa kwa usalama na amani katika eneo hilo.