Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 15, 2024 Local time: 09:38

Watu wawili wafariki kutokana na maporomoko ya ardhi, Switzerland


Picha ya angani ikionyesha maporomoka ya ardhi kutokana na mvua kubwa nchini Switzerland.
Picha ya angani ikionyesha maporomoka ya ardhi kutokana na mvua kubwa nchini Switzerland.

Polisi wa Switzerland wamesema Jumapili kwamba watu wawili wamekufa, huku mwingine akitoweka, kufuatia mvua kubwa zilizosababisha maporomoko ya ardhi, kusini mashariki mwa taifa hilo.

Mvua kubwa zimeripotiwa kunyesha nchini humo mwishoni mwa wiki na kupelekea mamia ya watu kuondoka makwao, baada ya mto Rhone kuvunja kingo zake.

Kulingana na gazeti la kieneo la La Regione, waliokufa ni wanawake wawili, waliokuwa kwenye likizo. Vyombo vya dharura vinaendelea kutadhmini namna ya kuokoa watu 300 waliotoka kuhudhuria michuano ya soka mjini Peccia, huku wengine 70, wakiokolewa kutoka eneo la kitalii kwenye kijiji cha Mogno.

Hali mbaya ya hewa inasemekana kufanya shughuli za uokozi kuwa ngumu, huku baadhi ya barabara zikiwa hazipitiki, pamoja na kukatika kwa umeme. Mvua kubwa pia zilinyesha kusini mashariki mwa Switzerland wikiendi iliopita na kuuwa mtu mmoja, pamoja na kusababisha uharibifu mkuwa wa moundo msingi.

Forum

XS
SM
MD
LG