Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:02

Watu wavamia benki kuchukuwa fedha zao wenyewe Lebanon


Picha ya Maktaba: Wananchi wa Lebanon wakiwa katika maandamano ya kupinga benki kuzuia fedha zao hapo Agosti 11, 2022. (Picha ya AP/Hussein Malla)
Picha ya Maktaba: Wananchi wa Lebanon wakiwa katika maandamano ya kupinga benki kuzuia fedha zao hapo Agosti 11, 2022. (Picha ya AP/Hussein Malla)

Hali ya taharuki katika benki ya Blom ya Lebanon, ilimalizika Jumatano, baada ya mwanamke aliyekuwa na bunduki akiwa na wenzake kuondoka katika benki na kiasi cha dola za kimarekani 13, elfu kutoka kwenye akaunti yake mwenyewe chanzo kutoka kundi la watetezi wa wateja wa shughuli za kibenki kimeeleza.

Sakata hilo na mengine yametokea baada ya walioweka fedha zao benki kwa takriban miaka mitatu na kushushwa thamani kukasirishwa na kuchukua uamuzi wa kuvamia benki hii ni kufuatia kuanguka kwa uchumi.

Sali Hafiz alirusha tukio lake moja kwa moja katika mitandao ya kijamii katika tawi la Beirut la benki ya Blom, ambapo alisikika akiwapigia kelele wafanyakazi wa benki kutoa fedha zake huku mlango wa benki ukiwa umefungwa.

Hafiz baadaye aliiambia televisheni ya Al Jadeed ya nchini humo kwamba bunduki haikuwa halisi na kwamba alikuwa anachukuwa fedha kwa ajili ya kumtibu dada yake anayeugua saratani. Amesema

“Sina cha kupoteza na nimefika mwisho. Siku mbili zilizopita, nilikwenda kwa meneja wa tawi na kumwambia dada yangu anakufa na hana muda. Baada ya kunipa wakati mgumu mwishso akasema watanipatia dola 200 kwa mwezi ambazo hazitoshi kununua hata sindano inayo hitajika kwa dada yangu kila siku. Ni aibu kusema hivi, ilifikia hatua nilikuwa tayari kuuza figo langu ili dada yangu apate matibabu. Sikuona faida ya kuishi wakati dada yangu anakufa mbele ya macho yangu.”

Chanzo kutoka chama cha wanaoweka fedha benki ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba chama chao kinawajibika kwa tukio hilo. Ibrahim Abdallah wa chama cha waweka fedha kwenye benki amesema.

“Kilichotokea ni kwamba Sali Hafiz alitaka fedha zake alizoweka kwenye benki ili amtibie dada yake saratani, na benki ikakataa kumpatia fedha zake. Kifupi alikwenda pale na akafunga benki kutoka kwa wafanyakazi na akachukua fedha zake mwenyewe.”

Hafiz mwenye umri wa miaka 28 na mbunifu wa ndani katika majumba amesema alifanikiwa kuchukuwa dola 13,000 kati ya dola 20,000 ambazo familia yake iliziweka benki. Amesema matibabu ya saratani kwa ajili ya dada yake yanagharama ya dola elfu 50.

Pia leo hii, mtu mmoja alivamia benki katika mji wa Aley uliopo kaskazini mashariki mwa Beirut limesema shirika la habari la taifa NNA.

Alikamatwa kwa mujibu wa NNA, lakini haikuelezwa kama mtu huyo alifanikiwa kuondoka na fedha zozote.

Mwezi uliopita, mtu mmoja alipata huruma kubwa baada ya kuvamia benki ya Beirut akiwa na bunduki na kuwaweka mateka wafanyakazi na wateja kwa saa kadhaa akitaka apewe kiasi cha fedha zake dola laki mbili zinazo shikiliwa ili kulipia matibabu ya baba yae anaye ugua.

Benki za Lebanon zimewazuia watu walio weka fedha zao benki kuzichukuwa toka kutokea mdororo wa kifedha miaka mitatu iliyopita, na kuacha wengi wa watu kushindwa kulipia mahitaji muhimu, na serekali imeshindwa kushughulikia jambo hili.

Lebanon imekuwa ikikabiliana na hali mbaya ya kudorora kwa uchumi toka mwaka 2019. Sarafu ya nchi hiyo imeshuka thamani yak kwa zaidi ya asilimia 90 hata kwenye masoko ya magendo huku kiwango cha umasikini na kukosekana kwa ajira kukikua kwa kasi.

XS
SM
MD
LG