Kamishna Msaidizi wa Lasbela Hamza Anjumk aliliambia gazeti la Dawn, la Pakistan, Kutokana na mwendo kasi, basi hilo liligonga nguzo ya daraja alipokuwa akigeuza kurudi upande mwingine karibu na Lasbela. Baadaye gari hilo lilizama kwenye korongo na kisha kuwaka moto.
Pia siku ya Jumapili, watoto 10 walifariki dunia wakati mashua yao ilipopinduka katika ziwa la Tanda Dam kaskazini magharibi mwa Pakistan, maafisa walisema.
Gazeti la The Dawn linaripoti kuwa watoto 17 na mwalimu mmoja waliokolewa na kwamba watoto wanne kati ya hao wako katika hali mbaya.