Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 06, 2024 Local time: 09:48

Watu wasiopungua 13 wauwawa katika mashambulizi matatu ya anga ya Israel


Moshi ukifuka kutoka kwenye jengo lililoshambuliwa na Israel huko Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza Julai 20, 2024. (Eyad BABA / AFP)
Moshi ukifuka kutoka kwenye jengo lililoshambuliwa na Israel huko Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza Julai 20, 2024. (Eyad BABA / AFP)

Watu wasiopungua 13 waliuawa katika mashambulizi matatu ya anga ya Israel yaliyopiga kambi za wakimbizi katikati mwa Gaza usiku wa kuamkia  Jumamosi

Watu wasiopungua 13 waliuawa katika mashambulizi matatu ya anga ya Israel yaliyopiga kambi za wakimbizi katikati mwa Gaza usiku wa kuamkia Jumamosi, kwa mujibu wa maafisa wa afya wa Palestina, huku mazungumzo ya kusitisha mapigano mjini Cairo yakionekana kupata maendeleo.

Miongoni mwa waliofariki katika Kambi ya Wakimbizi ya Nuseirat na Kambi ya Wakimbizi ya Bureij ni watoto watatu na mwanamke mmoja, kwa mujibu wa timu za ambulensi za Palestina ambazo zilisafirisha miili hiyo hadi hospitali ya karibu ya Al-Aqsa Martyrs. Maiti hizo 13 zilihesabiwa na waandishi wa habari wa AP katika hospitali hiyo.

Majeruhi wa hivi karibuni wanafuatia wakati adhimu wa matumaini katika vita vilivyoikumba Gaza, baada ya timu ya madaktari kumpata mtoto aliye hai kutoka kwa mama yake mjamzito wa Kipalestina aliyeuawa katika shambulizi la anga lililopiga nyumba yake huko Nuseirat jioni ya Alhamisi.

Forum

XS
SM
MD
LG