Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 02:02

Watu wanne wafariki kwenye mkanyagano wakati wa sherehe za Mashujaa nchini Kenya


Wanafunzi wakicheza wimbo wa kimaasai wakati wa sherehe za Mashujaa ya Kenya. Picha ya maktaba.
Wanafunzi wakicheza wimbo wa kimaasai wakati wa sherehe za Mashujaa ya Kenya. Picha ya maktaba.

Mkanyagano nchini Kenya wakati wa sherehe za maadhimisho ya sikukuu ya  kila mwaka ya Mashujaa umesababisha vifo vya takriban watu wanne Ijumaa, na kujeruhi wengine 100, ripoti zimesema.

Tukio hilo lilishuhudiwa baada ya mamia ya watu kunga'anga'nia kuingia katika kwenye uwanja wa michezo wa mji wa Kericho, magharibi mwa Kenya, ambako sherehe hizo zilikiuwa zikifanyikia,polisi imesema.

Rais William Ruto ambaye alihutubia maelfu ya watu katika uwanja huo takriban saa nne baadaye, hakuzungumzia kuhusu mkanyagano huo. Badala yake alielekeza hotuba yake katika mipango yake ya mabadiliko ya huduma za afya . Haikuwa bayana kama Ruto alikuwa anafahamu kuhusu mkanyagano huo uliotokea alipokuwa akitoa hotuba yake.

Saa chache kabla ya kuanza kwa sherehe hizo, mkuu wa mawaziri ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje, Musalia Mudavadi alimpokea rais wa Angola Joao Lourenco pamoja na mke wake Ana Dias Lourenco.

Hata hivyo Lourenco ambaye alikuja kwa ajili ya sherehe hizo hakuwepo uwanjani katika hafla hiyo iliyosifiwa na Ruto pamoja na maafisa wake wakuu serikalini.

Badala yake aliwakilishwa na balozi Antonio Tele ambaye hakueleza sababu za rais kutokuwepo.

Forum

XS
SM
MD
LG