Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 12, 2024 Local time: 00:14

Watu milioni 68 Kusini mwa Afrika wanateseka kutokana na ukame unaosababishwa na El Nino

Sehemu ya chini ya shimo la kunyweshea mifugo huko Mudzi, Zimbabwe Julai 2,2024 ambako ukame unaosababishwa na El Nino unaathiri mamilioni ya watu, na watoto wako hatarini zaidi. (Picha ya AP/Aaron Ufumeli)

Takriban watu milioni 68 Kusini mwa Afrika wanateseka kutokana na ukame unaosababishwa na El Nino ambao umeangamiza mazao katika kanda mzima, jumuiya ya kikanda ya SADC ilisema Jumamosi.

Ukame huo ulioanza mwanzoni mwa mwaka 2024, umeathiri uzalishaji wa mazao na mifugo, na kusababisha uhaba wa chakula na kuharibu uchumi mkubwa zaidi.

Wakuu wa nchi kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika yenye nchi 16 (SADC) walikuwa wanakutana katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare kujadili masuala ya kikanda ikiwa ni pamoja na usalama wa chakula.

Forum

XS
SM
MD
LG