Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 07:40

Watu elfu 30 wakadiriwa kuwa na MPOX Afrika


FILE PHOTO: Mpox survivors return home after recovering in Kinama zone, in Bujumbura
FILE PHOTO: Mpox survivors return home after recovering in Kinama zone, in Bujumbura

Takriban watu elfu  30 wameripotiwa kuwa na ugonjwa wa MPOX huko Afrika hadi sasa mwaka huu, wengi wao  wanatokea jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambako vipimo vimefanyika, shirika la afya  duniani WHO limesema leo.

Zaidi ya watu 800 wamekufa wakihofiwa kuwa na MPOX kote katika bara hilo wakati huo , WHO imeongeza kusema katika ripoti yake. Nchi jirani na Congo ya afrika ya kati, Burudi pia imeathiriwa na MPOX.

Taarifa zinasema MPOX inaweza kuenea haraka kwa njia ya mawasiliano ya mwili kugusana .

Kwa kawaida ugonjwa wenyewe unaanza taratibu lakini katika kesi nyingine hubadilika na kuwa na athari zaidi.

Kwa kawaida husababisha dalili zinazofanana na mafua na vidonda vilivyojaa usaha mwilini.

Taarifa ya WHO haikutoa takwimu linganishi za miaka iliyopita.

Hata hivyo shirika la afya ya umma la umoja wa Afrika limesema kesi 14, 957 na vifo 739 ziliripotiwa kutoka majimbo saba yaliyoathiriwa mwaka 2023 ikiwa ni ongezeko la asilimia 78.5 la kesi mpya kutoka mwaka 2022.

Forum

XS
SM
MD
LG