Wapiga mbizi wanendelea kukagua meli ya abiria ya Costa Concordia, na maeneo ya karibu ya meli hiyo kutafuta watu walokwama ndani ya meli hiyo iliyopunduka baada ya kwenda mrama karibu na kisiwa kidogo cha Giglio.
Mkuu wa kazi za uwokozi anasema hawawezi kuthibitisha idadi ya walopotea kutokana na hali ya taharuku ilyopo kutokana nna ajali hiyo. Hata hivyo walinzi wa pwani wanakadiria watu 70 wamepotea.
Abiria mmoja aliambia vyombo vya habari kwamba walikua wajitayarisha kwa chakula cha usiku waliposikia kishindo kikubwa kabla ya meli hiyo, Costa Concordia, kutikisika na kusimama na taa kuzimika.
Kulikuwepo na zaidi ya abiria na wafanyakazi 4,000 ajali hiyo ilipotokea Ijumaa usiku, na abiria kusema mtaharuku ulikuwa sawa na vile inaonekana kwenye filamu ya kuzama kwa meli ya Taitanic.