Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 08:20

Watu 64 wamefariki kwa ajali ya meli Madagascar


Mfano wa ajali za majini
Mfano wa ajali za majini

Meli hiyo ni meli ya mizigo ambayo haikuidhinishwa kusafirisha watu na ilijaza kupita kiasi na maji yalijaa kwenye injini alisema Mamy Randrianavony  mkurugenzi wa operesheni za bahari kwenye shirika la Maritime and River Port (APMF)

Watu 64 wamefariki katika ajali ya meli kwenye ufukwe wa kaskazini-mashariki mwa Madagascar na msako unaendelea kuwatafuta abiria 24 ambao hawajulikani walipo shirika la usafiri wa majini lilisema Jumatano.

Watu 50 walionusurika walipatikana shirika la Maritime and River Port lilisema. Meli hiyo ni meli ya mizigo ambayo haikuidhinishwa kusafirisha watu na ilijaza kupita kiasi na maji yalijaa kwenye injini alisema Mamy Randrianavony mkurugenzi wa operesheni za bahari kwenye shirika la Maritime and River Port (APMF).

Meli ilizama Jumatatu usiku ikiwa na watu 138 kulingana na maelezo ya APMF.

XS
SM
MD
LG