Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 06:43

Watu 6 wauawa katika mashambulizi ya Russia kwenye miji tofauti ya Ukraine


Majengo yaliyoharibiwa na mashambulizi ya Russia mjini Kyiv, Machi 18, 2022. Picha ya AP
Majengo yaliyoharibiwa na mashambulizi ya Russia mjini Kyiv, Machi 18, 2022. Picha ya AP

Watu 6 wameuawa na mashambulizi ya Russia katika mji mkuu wa Ukraine na mkoa wa mashariki wa Sumy, maafisa wa Ukraine wamesema Jumatatu, baada ya darzeni ya ndege zisizokua na rubani maarufu drones kuushambulia mji wa Kyiv.

Maafisa wa Ukraine wamesema ndege hizo zilitengenezwa na Iran, ambazo zimetumiwa na Russia kuendesha mashambulizi yaitwayo Kamikaze ambapo ndege hizo hulipuka baada ya shambulio.

Rais Volodymyr Zelensky amesema katika ujumbe wa Telegram “ Usiku kucha na asubuhi, adui amefanyia vitisho raia. Drones za Kamikaze na makombora yanaishambulia Ukraine. Adui anaweza kuishambulia miji yetu lakini hataweza kutuvunja moyo,’’ Zelensky amesema.

Meya wa Kyiv Vitali Klichko amesema miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa ni wilaya ya Shevchenko, eneo lilioshambuliwa kwa makombora ya Russia wiki iliyopita.

Ubalozi wa Marekani mjini Kyiv umeyataja mashambulizi hayo dhidi ya raia kuwa ya “kukata tamaa na ya kulaaniwa.”

XS
SM
MD
LG