Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 02:37

Watu 6 wameuwawa Ukraine na shambulizi la Russia


Takriban watu sita wamejeruhiwa Jumatatu, baada ya nyumba, magari na biashara kuharibiwa na mabomu matatu yaliyorushwa na Russia, kwenye mji wa kaskazini mashariki mwa Ukraine wa Kharkiv, meya wa jiji hilo Ihor Terekhov, amesema kupitia mtandao wa Telegram.

Meya Terekhov, amesema huenda bado kuna watu chini ya vifusi kufuatia shambulizi katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine.

Kharkiv na mji jirani kwa muda mrefu imelengwa na mashambulizi ya Russia, lakini kwa siku za karibuni mashambulizi yamekuwa makali zaidi yakiwalenga raia na mtandao wa nishati wa eneo hilo.

Russia, inakanusha kuwalenga raia kwa makusudi, lakini maelfu ya raia tayari wameuwawa na kujeruhiwa katika kipindi cha uvamizi wake kwa Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG