Wakati huohuo takriban watu 16 wamejeruhiwa wengi wao wakiwa katika hali mbaya. Ajali hiyo imehusisha basi la abiria na na lori la mizigo yaliyogongana kilomita 200 kutoka mji mkuu Nairobi.
Kwa mujibu wa afisa mkuu wa idara ya usalama barabarani, Bonde la Ufa, Zero Arome ajali hiyo ilitokea majira ya saa tisa alfajiri.
Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya limeripiti ajali hiyo katika akaunti yake ya Tweeter, likisema majeruhi wamepelekwa katika Hospitali za Nakuru Level Five na ile ya Molo Sub-County.
Mapema mwezi Disema 2017 zaidi ya watu 20 walipoteza maisha katika ajali nyingine mbaya katika eneo hilo hilo.