Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:58

Watu 23 wauawa Syria


Maelfu ya waandamanaji wa Syria katika mkutano wa hadhara, Julai 28, 2011
Maelfu ya waandamanaji wa Syria katika mkutano wa hadhara, Julai 28, 2011

Serikali ya Syria yaendelea kuuwa waandamanaji

Wanaharakati na mashahidi nchini Syria wanasema vifaru vya kijeshi viliingia katika mji wa katikati wa Hama mapema Jumapili na kuuwa watu 23. Walioshuhudia wanasema kulikuwa na mapigano makali ya risasi mjini Hama mji ambao katika siku za karibuni umekuwa kitovu cha maandamano dhidi ya rais Bashar al-Assad. Wanaharakati wanasema bwana Bashar anajaribu kuzima maandamano ya amani ambayo yalianza mwezi Machi kupinga utawala wake wa miaka 11. Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema vikosi vya Syria vimeuwa raia 1,600 tangu ukamataji wa waandamanaji kuanza. Serikali inawalaumu magaidi na wanamgambo kwa ghasia hizo ikidai kuwa wameuwa mamia ya maafisa wa ulinzi. Imekuwa vigumu kuthibitisha ukweli juu ya ghasia za Syria kwa sababu serikali imepiga marufuku waandishi habari wa kigeni kuripoti juu ya matukio nchini humo.

XS
SM
MD
LG