Boti hiyo iliyokuwa imebeba watu 47, ilipinduka siku ya Jumamosi katika bahari ya Ankazomborona kaskazini mwa Madagascar, mamlaka ya Bahari na Mito lilisema katika taarifa.
Shirika hilo limesema boti hiyo ilipata ajali, ambapo 23 kati ya waliokuwemo waliokolewa, huku miili 22 ikipatikana. Wengine wawili bado walikuwa hawajulikani waliko.
Afisa wa polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema wengi wa waliookolewa walikimbia ili kuepuka kukamatwa kwa kujaribu kusafiri hadi Mayotte.