Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:01

Watu 203 wauawa na jeshi la Mali, uchunguzi waitishwa


Wanajeshi wa Mali wakipiga doria katikati mwa Mali. Feb. 28, 2020. PICHA: AFP
Wanajeshi wa Mali wakipiga doria katikati mwa Mali. Feb. 28, 2020. PICHA: AFP

Ufaransa imesema kwamba ina wasiwasi mkubwa kutokana na kile imetaja kama ukiukwaji mkubwa na mauaji yaliyofanywa na wanajeshi wa Mali, wakishirikiana na mamluki wa kundi la Wagnar kutoka Russia.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema kwamba ina wasiwasi kuhusu ripoti za kuwepo ukiukwaji wa haki za raia dhidi ya wakaazi wa vijiji vya Moura, uliotekelezwa na wanajeshi wa Mali na mamluki hao, na kupelekea vifo vya maelfu ya raia.

Jeshi la Mali limesema kwamba limeua wapiganaji 203 kutoka makundi yenye silaha, na kuyataja kuwa makundi ya kigaidi, wakati wa oparesheni katika eneo la Saheli, katikati mwa Mali, kati ya March tarehe 23 na 31.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetoa taarifa, na kusema kwamba Marekani inafuatilia kwa karibu sana ripoti hizo zinazokera kwamba idadi kubwa ya watu waliuawa katika sehemu za vijijini katikati mwa Mali.

Ufaransa inataka uchunguzi kuanzishwa kwa haraka kuhusiana na tukio hilo, na kuwafungulia mashtaka wahusika.

XS
SM
MD
LG