Takriban watu 200 wamefariki nchini Vietnam ikiwa ni matokeo ya kimbunga Yagi, na wengine 128 hawajulikani walipo wakati mafuriko na maporomoko ya ardhi yalipotokea.
Gazeti la VNExpress la Vietnam limeripoti Alhamisi kuwa watu 199 wamefariki huku wengine zaidi ya 800 wamejeruhiwa. Katika mji mkuu, maji ya mafuriko kutoka Red River yalipungua kidogo lakini maeneo mengi bado yalikuwa yamejaa maji katika baadhi ya maeneo.
Idadi ya vifo iliongezeka mapema wiki hii wakati mafuriko ya ghafla yalipoukumba mji mzima wa Lang Nu, katika jimbo la Lao Cai kaskazini mwa Vietnam siku ya Jumanne.
Mamia ya wafanyakazi wa uokoaji walifanya kazi bila kuchoka siku ya Jumatano kuwatafuta manusura, lakini hadi kufikia leo Alhamisi asubuhi wanakijiji 53 bado hawajulikani waliko.
Forum