Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 11:07

Raia 19 wauawa kwenye shambulizi Mogadishu, Somalia


Maafisa wa usalama wamkamata mshukiwa aliyeokolewa ndani ya mgahawa wa Pizza House, mjini Mogadishu, Somalia tarehe 15, Mei, 2017.
Maafisa wa usalama wamkamata mshukiwa aliyeokolewa ndani ya mgahawa wa Pizza House, mjini Mogadishu, Somalia tarehe 15, Mei, 2017.

Hali ilitulia Alhamisi jioni kwenye mgahawa mmoja mjini Mogadishu, baada vikosi vya Usalama nchini Somalia, kuwashinda nguvu wanamgambo wa Al-Shabaab baada ya mapigano yaliyoendelea kwa takriban saa kumi na moja.

Maafisa wa serikali waliiambia Sauti ya Amerika kwamba raia wasiopungua 19 waliuawa kwenye shambulizi hilo lililoanza Jumatano jioni kwa mlipuko wa bomu la kwenye gari, uliotokea nje ya migahawa miwili iitwayo Pizza House na Posh Treats na kusababisha uharibifu mkubwa.

Walioshuhuduia walisema kuwa watu waliokuwa na bunduki waliingia kwenye migahawa hiyo miwili na kupambana vikali na vikosi vya usalama.

Mkuu wa polisi mjini Mogadishu Meja Abdifatah Bashir Ali, aliiambia Sauti ya America kwamba vikosi maalum vilianzisha operesheni kubwa muda mfupi kabla ya saa 12 asubuhi ya Alhamisi na waliweza kuwashinda nguvu washambuliaji hao baada ya mapambano yaliyochukua saa 11.

XS
SM
MD
LG