Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 15:55

15 wauwawa katika mlipuko wa bomu Somalia


Gari la wagonjwa likibeba wagonjwa baada ya shambulizi kuelekea Madina Hospital mjini Mogadishu Somalia June 15, 2021. REUTERS/Feisal Omar
Gari la wagonjwa likibeba wagonjwa baada ya shambulizi kuelekea Madina Hospital mjini Mogadishu Somalia June 15, 2021. REUTERS/Feisal Omar

Watu wasiopungua 15 waliuawa Jumanne katika shambulizi la kujitoa muhanga kwenye kambi ya kijeshi katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, shahidi ameliambia shirika la habari la Reuters na kusema alihesabu miili hiyo katika Hospitali ya Madina alisema.

Maafisa wa hospitali hiyo walithibitisha kwamba waliokufa waliuawa katika shambulizi la mapema asubuhi katika kambi ya jeshi. Hakukuwa na madai ya mara moja ya aliyehusika. Kundi la wanamgambo wa Kiislam la al-Shabaab mara nyingi hufanya mashambulizi ya mabomu katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Afisa wa jeshi la Somalia, Odawaa Yusuf Rage, aliwaambia wanahabari wa serikali mapema Jumanne kuwa waajiriwa wapya 10 waliuawa, na wengine 20 walijeruhiwa, wakati mshambuliaji wa kujitoa muhanga alipotegua milipuko katika kizuizi nje ya kambi ya mafunzo ya kijeshi ya General Degaban katika mji mkuu.

XS
SM
MD
LG