Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:05

Watu 14 wauawa katika kambi ya waliokoseshwa makazi kaskazini mashariki mwa DRC.


DRC map, North Kivu province
DRC map, North Kivu province

Raia 14 wakiwemo watoto saba waliuawa katika kambi ya watu wasiokuwa na makazi huko kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), shirika la Msalaba Mwekundu katika eneo lilisema Jumapili.

Watu wazima saba na watoto saba akiwemo mtoto mmoja wa miaka miwili wote waliuawa katika shambulizi la mapanga siku ya Jumamosi katika eneo la Ituri kulingana na orodha ya Msalaba Mwekundu ambayo shirika la habari la AFP iliiona.

Jean D’Zba Banju kiongozi wa jamii katika eneo la Djugu huko Ituri alisema wanamgambo wa CODECO waliingia Drakpa ambako waliwaua watu 12 kwa mapanga.

Wanamgambo wa CODECO waliingia Drakpa na kuanza kuwakata watu kwa mapanga. Hawakufyatua risasi ili waweze kufanya operesheni kwa utulivu Banju aliiambia AFP.

Waathirika ni watu wasiokuwa na makazi ambao walikimbia kutoka kijiji cha Ngotshi na kuweka makazi yao huko Drakpa alisema, akiongeza kuwa watu watano wengine walijeruhiwa.

CODECO ni kundi la kisiasa na kidini ambalo linadai kwamba linawakilisha maslahi ya kundi la kabila la wa Lendu.

XS
SM
MD
LG