Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 06, 2024 Local time: 03:11

Watu 121 wamefariki katika mkanyagano India


Waombolezaji baada ya vifo kutokana na mkanyagano wa watu India, July 2, 2024.
Waombolezaji baada ya vifo kutokana na mkanyagano wa watu India, July 2, 2024.

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mkanyagano kwenye mkusanyiko wa kidini wa kihindu katika jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh nchini India, imefikia watu 121.

Hakimu wa wilaya Ashish Kumar, amewaambia waandishi wa habari kwamba tukio limetokea katika kijiji kilichopo kiasi cha kilomita 200 kusini mashariki mwa mji mkuu wa india, New Delhi.

Kundi kubwa la watu lilikuwa linaharakisha kuondoka kwenye hafla inayojulikana kama Satsang, iliyokuwa imeandaliwa na kiongozi wa kidini Bhole Baba.

Ripoti ya polisi inasema kwamba uchunguzi wa awali unasema karibu watu 250,000 walikuwa wameingia katika hema la muda ambapo hafla ilifanyika. Maafisa walikuwa wameruhusu watu 80,000 pekee kuhudhuria hafla hiyo.

Ripoti kadhaa zinasema kwamba mkanyagano ulianza pale waumini walipoanza kumfuata Bhole Baba kutoka kwenye hema hilo, wakati alipokuwa anaondoka.

Idadi kubwa ya watu waliteleza kwenye matope na kuanguka kwenye mtaro uliokuwa na maji, na wengi walikufa kutokana na kuangukiwa na wengine ndani ya mtaro huo wenye maji. Idadi kubwa ya waliofariki ni watoto na akina mama. Darzeni kadhaa wamejeruhiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG