Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:47

Watu 11 wauawa katika shambulizi la waasi kaskazini mashariki mwa Congo


Waasi wa M23 wakisimama na silaha zao wakati wa hafla ya kuanza kuondoka katika maeneo wanayodhibiti katika mji wa Kibumba, mashariki mwa DRC, Disemba 23, 2022.
Waasi wa M23 wakisimama na silaha zao wakati wa hafla ya kuanza kuondoka katika maeneo wanayodhibiti katika mji wa Kibumba, mashariki mwa DRC, Disemba 23, 2022.

Kundi la waasi limeua watu 11 kaskazini mashariki mwa Congo, afisa wa eneo hilo amesema Jumapili.

Isaac Kibira, naibu mkuu wa mtaa wa Bwito katika mkoa wa Kivu Kaskazini, amesema watu hao waliuawa na waasi wa M23.

Miili ya raia 11 ilipatikana Jumapili asubuhi, iliachwa kwenye safu mbili kwenye nyasi.

Waasi wa M23 walikuwa wanadhibiti eneo hilo tangu siku ya Jumanne kabla ya kuondoka, kulingana na kundi la utafiti la Sahel Intelligence lenye makao yake mjini Paris.

Kundi la M23 halikupatikana mara moja kutoa maelezo juu ya madai hayo.

M23 ni moja kati ya makundi 120 yenye silaha yanayopigana mashariki mwa Congo, mengi kati ya hayo yakipigania umiliki wa ardhi na udhibiti wa migodi ya madini yenye thamani, huku makundi mengine yakijaribu kulinda jamii zao dhidi ya makundi hasimu yenye silaha.

M23 walipodhibiti eneo la Bwito wiki iliyopita ilisababisha mamia ya watu kuhama makazi yao na kukimbilia katika jamii jirani, na kuongeza kile ambacho Umoja wa Mataifa unakadiria ni watu milioni 5.5 wakimbizi wa ndani kutokana na machafuko.

Forum

XS
SM
MD
LG