Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 28, 2024 Local time: 22:50

Watu 1,300 wapoteza maisha wakati wa Hija


Zaidi ya watu 1,300 wamefariki dunia wakati wa ibada ya Hija mwaka huu nchini Saudi Arabia huku waumini wakikabiliwa na hali ya joto kali katika maeneo matakatifu ya Kiislamu katika ufalme huo wa jangwani, serikali ya Saudi imetangaza Jumapili.

Waziri wa Afya wa Saudia, Fahd bin Abdurrahman Al-Jalajel, amesema kuwa asilimia 83 ya vifo hivyo, ni mahujaji ambao hawakuidhinishwa waliotembea umbali mrefu katika hali ya joto inayoongezeka, kushiriki ibada ya Hija ndani na karibu na mji mtakatifu wa Mecca.

Akizungumza na televisheni inayomilikiwa na serikali, waziri huyo amesema mahujaji 95 walitibiwa hospitalini, huku baadhi yao wakisafirishwa kwa ndege kwa matibabu zaidi katika mji mkuu wa Riyadh.

Amesema mchakato wa kuwatambua watu hao ulichelewa kwa sababu ya kutokuwepo kwa vitambulisho kwa mahujaji wengi waliofariki dunia.

Forum

XS
SM
MD
LG