Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 17:31

Vijana 4 zaidi waokolewa kutoka pangoni Thailand


Madaktari wa huduma ya kwanza wakiwa wamembeba mtoto kumuingiza katika helikopta ili kumpeleka huko Chiang Rai, Thailand, July 8, 2018
Madaktari wa huduma ya kwanza wakiwa wamembeba mtoto kumuingiza katika helikopta ili kumpeleka huko Chiang Rai, Thailand, July 8, 2018

Angalau vijana watano kati ya kumi na mbili na kocha wao wameokolewa baada ya kuwa wamekwama katika pango lililokumbwa na mafuriko kwa zaidi ya wiki mbili.

Habari zilizokuwa hazijaweza kuthibitishwa zinaeleza kuwa watoto watatu zaidi wameokolewa Jumatatu.

Watoto wanne wa kwanza, waliokolewa na wazamiaji Jumapili, ambao walichukuliwa wa usafiri wa anga kupelekwa kwenye hospitali ya Chiang Rai, na watano, alitolewa kutoka katika pango siku ya Jumatatu, na anatarajiwa kuungana nao baada ya matibabu ya mwanzoni katika hospitali iliyoko karibu na mapango ya Tham Luang caves.

Lakini mpaka sasa familia za vijana hao hazijafahamishwa ni vijana gani kati yao waliokuwa wameokolewa.

Waziri wa Mambo ya Ndani Anupong Paojina amesema wazamiaji hao hao walioshiriki katika shughuli za uokozi Jumapili wanafanya operesheni hiyo tena Jumatatu kwa sababu sasa wanauzoefu na hali iliyoko katika pango hilo.

Kikundi hicho cha vijana na kocha wao wamekwama takriban kilomita nne ndani ya pango hilo.

XS
SM
MD
LG