Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 10:47

Watanzania waanza kupiga kura


Watanzania wapiga kura
Watanzania wapiga kura

Watanzania walianza kupiga kura kote nchini Jumatano asubuhi kuchagua rais, wabunge na madiwani baada ya vituo kufunguliwa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na visiwani Zanzibar.

Hii ni kufuatia takriban miezi miwili ya kampeni ambazo ziliwavutia raia wengi, wakiwasikiliza wagombea wakijieleza na kunadi sera zao.

Takriban wapiga kura 29.75 wamejiandikisha kwa zoezi hilo, ambapo kati ya hao, 566, 352 wamejiandikisha visiwani Zanzibar.

Tume ya uchaguzi imeeleza kwamba kura zitaanza kuhesabiwa Jumatano usiku baada ya vituo kufungwa.

Rais wa sasa John Pombe Magufuli anakabiliwa na ushindani kutoka kwa wagombea 15 akiwemo mpinzani mkuu Tundu Lissu mwenye umri wa miaka 52, anayegombea urais kwa tiketi ya chama cha upinzani – Chadema.

Visiwani Zanzibar wagombea wakuu wa urais ni Huseein Mwinyi wa CCM na Maalim Seif Sharif Hamad wa Chadema.

Aidha vyama mbalimbali kote nchini vina wagombea wao wa ubunge na udiwani.

Waandishi wa Sauti ya Amerika waliendelea kutembelea vituo mbalimbali na kutuma ripoti zao ili kupeperushwa kwa njia ya redio, televiseni na mtandao wa internet.

Wasikilizaji wa idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika wanashauriwa kufuatilia matukio kama yanavyotokea moja kwa moja kwa kutembelea kurasa za Voaswahili za Facebook, Instagram na Twitter, kando na kusikililiza matangazo ya redio na televisheni.

Mengine yatafuata...

XS
SM
MD
LG