Takriban watu 81 wameuawa nchini Iran mwezi Agosti pekee, kiasi kikubwa zaidi ya 45 walioripotiwa mwezi Julai, kundi la wataalam 11 huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema katika taarifa.
Idadi iliyoripotiwa ya walionyongwa toka kuanza kwa 2024 imeongezeka na kuwa zaidi ya 400, pamoja na ya wanawake 15, wamesema.
“Tuna wasiwasi mkubwa na ongezeko hili kubwa la mauaji,” wamesema wataalam hao, ambao wameteuliwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lakini hawazungumzi kwa niaba ya Umoja wa Mataifa.
Forum