Wametaja hatua hiyo kuwa itaziwezesha nchi zao kudhihirisha uwezo wao wa maendeleo ya kiuchumi, huku wakisisitiza kujitolea kwa nchi zao kuleta mtazamo mpya katika utaratibu wa ushirikiano kwa kutumia faida zao za kipekee.
Pia wataalamu hao wamesisitiza kujitolea kwa nchi zao kuleta mtazamo mpya katika utaratibu wa ushirikiano kwa kutumia faida zao za kipekee.
Saudi Arabia, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Iran na Ethiopia ni wanachama rasmi wa BRICS kuanzia Jumatatu.
Mtaalamu wa masuala ya mawasilaino wa Misri alielezea matarajio ya muda mrefu ya Misri ya kujiunga na utaratibu wa ushirikiano wa BRICS na matarajio yake ya kuhimiza matumizi ya sarafu za ndani katika biashara ya kimataifa,
Pia ameeleza matarajio ya nchi yake kutumia miamala ya kifedha kati ya nchi za BRICS na washirika wao wa kibiashara chini ya utaratibu wa ushirikiano.
Mtaalamu huyo aidha alisisitiza kuwa hatua hii itachangia katika kuleta mageuzi katika mifumo ya fedha ya kimataifa, kuongeza uwakilishi na sauti ya nchi zinazoendelea, na kusukuma mfumo wa fedha wa kimataifa kuelekea mabadiliko mchanganyiko.
Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.
Forum