Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:54

Wataalam wa haki za binadamu wasema ukiukaji wa haki za binadamu umekithiri nchini DRC


Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu Volker Turk, akitembelea kambi ya watu waliohamishwa kwenye makazi yao ya Bulengo, karibu na Goma, Aprili 17,2024. Picha ya AFP
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu Volker Turk, akitembelea kambi ya watu waliohamishwa kwenye makazi yao ya Bulengo, karibu na Goma, Aprili 17,2024. Picha ya AFP

Wataalam wa haki za binadamu wanaonya kwamba hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imedorora sana kwa mara nyingine huku mapigano kati ya makundi yenye silaha, mashambulizi kwenye shule na hospitali, unyanyasi wa kingono na manyanyaso mengine yakikithiri.

Akianzisha mjadala kuhusu DRC kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu mjini Geneva, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu Volker Turk ameitaka Jumuia ya Kimataifa kujali hali ya raia wa Congo wanaoathiriwa na mchanganyiko wa ghasia zinazokithiri, maslahi ya kikanda na kimataifa, biashara ya utumwa na utawala dhaifu wa kisheria.

Alisema idadi ya waathirika wa ukiukaji wa haki za binadamu inazidi kuongezeka, huku makundi yenye silaha yanayopigana katika mikoa ya mashariki yakihusika zaidi katika ukiukaji huo, ikiwemo mashambulizi mabaya dhidi ya raia na miundombinu ya raia, ikiwemo shule na hospitali.

Alisema unyanyasaji wa kingono unaongezeka licha ya juhudi za kuuzuia na kuchunguza kesi za vitendo hivyo.

“Makundi yenye silaha yanateka watu, kuwaingiza wanawake na wasichana katika utumwa wa ngono. Wengi wao wameuawa baada ya kubakwa. Kesi hizi, bila shaka, hazijaripotiwa zote. Huu ni ukatili,” alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG