Makundi ya kutoa misaada yamesema kwamba kuna ongezeko kubwa la wakimbizi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab ambayo tayari inakabiliwa na ukosefu wa chakula.
Baadhi ya wakipizi wamepoteza Watoto wao walipokuwa njiari kuelekea Kenya kutafuta chakula.
Serikali ya Kenya iliweka marufuku ya kusajili wakimbizi wapya katika kambi hiyo ya Dadaab, karibu na Somalia, lakini shirika la kuwahudhumia wakimbizi la UNHCR limesema kwamba wakimbizi 80,000 waemingia nchini Kenya katika muda wa miezi michache iliyopita.
Mashirika ya kutoa msaada yanasema kwamba ongezeko la wakimbizi limepelekea ukosefu wa chakula cha kuwapa kambini.