Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 03, 2025 Local time: 06:42

Washirika na hasimu wa Marekani washutumu pendekezo la kuchua udhibiti wa Gaza


Picha inayoshukuru Rais wa Marekani Donald Trump kwenye jengo la hoteli mjini Tel Aviv, Februari 5, 2025.
Picha inayoshukuru Rais wa Marekani Donald Trump kwenye jengo la hoteli mjini Tel Aviv, Februari 5, 2025.

Washirika wa Marekani pamoja na mahasimu wake wote Jumatano wameshutumu pendekezo la rais wa Marekani Donald Trump kwamba Marekani ichukue udhibiti wa Gaza

Kando na hilo pia kuna wazo na kulazimisha zaidi ya Wapalestina milioni 2 kwelekea kwenye mataifa mengine na kisha kugeuza Gaza kuwa “Riviera ya Mashariki ya Kati.” Mapendekezo ya Trump yaliyotolewa mbele ya wanahabari kwenye Ikulu ya Marekani akiwemo Waziri Mkuu wa IsraeL Benjamin Netanyahu yalikuwa ya haraka na yenye utata kutoka kwa kiongozi huyo ambaye wakati mmoja alikuwa mfanyabiashara tajiri wa ujenzi na uuzaji wa majengo mjini New York.

Uingereza, China, Ujerumani, Ireland, Russia na Uhispania wote wamesema kuwa wanaendelea kuunga mkono suluhisho la mataifa mawili- yaani taifa huru la Kipalestina litakalojumuisha Gaza na eneo lililokaliwa la Ukingo wa Magharibi kupakana na Israel. Pendekezo la mataifa mawili linalolenga kumaliza miongo kadhaa ya vita na migogoro Mashariki ya Kati kwa muda mrefu limekuwa likiungwa mkono na sera za Marekani ingawa utawala wa Netanyahu umekuwa ukipinga.

Saudi Arabia, mshirika muhimu wa Marekani huko Mashariki ya Kati kupitia taarifa imesema kuwa msimamo wake wa uhuru wa nchi ya Palestina ni imara na wala hautabadilika. “Msimamo wa Australia ni ule ule tuliokuwa nao asubuhi, sawa na ilivyokuwa mwaka jana na muongo mmoja uliopita,” Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese alisema, akiunga mkono suluhisho la mataifa mawili.

Forum

XS
SM
MD
LG