Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 20:44

Washington ni mwenyeji wa mkutano wa wanachama wa NATO


Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa NATO akiwa katika makao makuu ya NATO huko Brussels. June 14, 2024.
Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa NATO akiwa katika makao makuu ya NATO huko Brussels. June 14, 2024.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema wanachama wote wa NATO wanataka amani na hilo linaweza kupatikana

Wakati NATO ikijiandaa kukutana Jumanne kwa mkutano wa siku tatu mjini Washington kwa maadhimisho ya miaka 75, muungano huo unaimarisha uungaji mkono wake kwa Ukraine katika vita vinavyoendelea na Russia.

Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumapili akitathmini maandalizi ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema wanachama wote wa NATO wanataka amani, na hilo linaweza kupatikana kama Rais wa Russia Vladimir Putin anaelewa hawezi kushinda kwenye uwanja wa vita.

Njia ya haraka ya kumaliza vita hivi ni kushindwa vita, alisema. Lakini hilo halitaleta amani. Hili litaleta ukaliaji kimabavu. Stoltenberg alielezea hatua muhimu ambazo NATO itachukua, ikijumuisha kuanzishwa kwa amri kamandi ya kijeshi nchini Ujerumani, kuimarisha misaada ya kifedha na kijeshi, na mikataba ya ulinzi ya pande mbili.

Forum

XS
SM
MD
LG