Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:00

Warepublican wa bunge la Marekani wanachunguza chanzo cha COVID-19


Speaker wa baraza la wawakilishi Kevin McCarthy akikula kiapo Januari 7, 2023
Speaker wa baraza la wawakilishi Kevin McCarthy akikula kiapo Januari 7, 2023

Warepublican, wanaodhibithi baraza la wawakilishi, wameanza uchunguzi kuhusu chanzo cha virusi vya Covid-19, kwa kutoa barua kadhaa kwa maafisa wa sasa na wa zamani wa utawala wa rais Joe Biden, wakiwataka kutoa ushahidi.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge inayosimamia utendaji kazi wa serikali kuu na kamati ndogo kuhusu janga la virusi vya Corona, wameomba taarifa kutoka kwa watu kadhaa, kwa kuzingatia dhana kwamba virusi vya Corona vilitoka kwa makossa kutoka maabara moja nchini China.

Kati ya wale ambao wametakiwa kutoa taarifa ni mtaalam wa magonjwa Dr. Anthony Fauci.

Wanasayansi wanasema kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba virusi vya Corona vilianza kwa Wanyama kabla ya kuambukiza binadamu.

Watafiti wa virusi hawajapata taaarifa zozote zinazohusiana na dhana kwamba huenda virusi vya Corona vilitengenezwa katika maabara.

XS
SM
MD
LG