Kura hiyo pia inaonekana kama mtihani kwa chama tawala cha waziri mkuu Fumio Kishida, ambacho kinaamunga mkono Koike, ambaye ni mwanamke wa kwanza kuongoza serikali ya Tokyo.
Mji huo wenye wakazi milioni 13.5 una ushawishi mkubwa wa kisiasa na kitamaduni, ukiwa na bajeti inayofanana na baadhi ya mataifa, huku ukiwa na umuhimu mkubwa kwenye siasa za Japan.
Nafasi ya kuongoza mji huo imewavutia jumla ya wagombea 55 akiwemo mwanamke mwingine wa kiliberali, aliyewahi kuwa mbunge, na anayeungwa mkono na vyama vya upinzani, huku akipendelea kutumia jina moja tu la Renho.
Baadhi ya masuala muhimu yaliyotawala kampeni za uchaguzi huo ni uchumi, uwezo wa kukabiliana na majanga, pamoja na idadi ndogo ya uzazi mjini Tokyo.
Forum